Friday May 18th 2012

Halmashauri Kongwa yanunua madawati 525

Na Fatma Gaffus,

Dodoma.

 

 

Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa mkoani Dodomaimenunua madawati 525 yenye thamani ya shilingi milioni 36.5 na kuyasambaza katika shule 53 za Msingi wilayani humo.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bwana Athman Akalama alisema lengo ni kupunguza tatizo la wanafunzi kukaa chini.

Afisa Elimu ya Msingi wa Wilaya ya Kongwa Bwana Ligola Michael alisema kati ya wanafunzi 55,848, wanaokaa kwenye madawati ni 29,841 na wengine 26,007 wanakaa chini.

Aidha alisema kiasi cha shilingi milioni 40 kimetumika kwa ajili ya ujenzi wa Maabara katika shule ya sekondari Zoissa.

Wilaya ya Kongwa ina shule za msingi 105 zenye wanafunzi 55,848.

Mahitaji ya madawati ni 18,616 na yaliyopo ni madawati 9,947 na upungufu ni madawati 8,669.

 

Mwisho.

3 Comments for “Halmashauri Kongwa yanunua madawati 525”

  • mussa ommary says:

    NAOMBA WILAYA YA KONGWA ICHUNGUZWE KWANI WAFANYAKAZI WENGI HAWANA SIFA HASA IDARA YA ELIMU KWAN WANASHINDWA KUWAJIBIKA ILA WANAWEZA KUKATA MISHAHARA YA WALIMU NDO FANI YAO.KWAN MATATIZO YA WALIMU NI MAKUBWA SANA.LAKINI HATA HAWASIKILIZI .JIBU FUATILIA MATOKEO YA MWAKA KATIKA WILAYA YA KONGWA NI UOZO MTUPU.NABADO KUGOMA SIO KUKAA BARABRANI///

  • mussa ommary says:

    SIO HIVYO TU WALIMU WENGI WAMEPANDISHWA MADARAJA MIAKA ZAIDI YA SABA MPAKA LEO HAWAJABADILISHIWA MISHAHARA YAO KWANINI? JIBU NI UFISADI ULIOKITHIRI KATIKA WILAYA YA KONGWA,LAKIN WAHUSIKA WAPO WANAUZA SURA NA KUPAKA PODA MAOFISINI.TUTAFIKA KWA PHILOSOPHY YA ARI YA ZAMANI,NGUVU YA ZAMAN,NA TUNASONGA NYUMA

  • mussa ommary says:

    MABOSI TUME YA UTUMISHI NI MAJINA TU KWANI HAWANA LOLOTE,MATOKEO YA SHULE ZA KATA MAARUFU KAMA KAYUMBA SEC SCHOOL YA KIDATO CHA NNE NI UOZO MTUPU NA BADO WATAFELI MPAKA WAKOME.SISI KAMA WALIMU TUTAENDELEZA KUFELISHA HADI PALE TUTAKAPOSIKILIZWA MATATIZO YETU.


Leave a Comment

More from category

TACAIDS yashauriwa kutenga fedha za miradi kwa waathirika.
TACAIDS yashauriwa kutenga fedha za miradi kwa waathirika.

Na Grace Semfuko,                                                    [Read More]

Tatizo la umeme, Serikali yahitaji mtaji mkubwa kuwekeza.
Tatizo la umeme, Serikali yahitaji mtaji mkubwa kuwekeza.

Na Fatma Gaffus, Dodoma. Serikali imesema kuwa inahitaji mtaji mkubwa ili ifanye uwekezaji  katika sekta ya umeme [Read More]

Siku ya familia, Mabadiliko ya kiuchumi bado changamoto.
Siku ya familia, Mabadiliko ya kiuchumi bado changamoto.

Na Neema Ndetto,          Dar es salaam. Utandawazi na mabadiliko ya kiuchumi duniani ni miongoni mwa [Read More]

Hati Miliki, Ubora wa maudhui changamoto katika mfumo wa digitali
Hati Miliki, Ubora wa maudhui changamoto katika mfumo wa digitali

Na Dennis Mwasalanga,          Dar Es Salaam.  Wakati mfumo wa utangazaji ukielekea katika mfumo wa digitali, [Read More]