Wednesday February 22nd 2012

CUF yapoteza wanachama 1,122 Ilemela.

Na Mwandishi wetu, Mwanza 

Wanachama 1,122 wa Chama cha Wananchi CUF wilayani Ilemela mkoani Mwanza wamejivua Uanachama kwa madai kuwa chama hicho kina ombwe la uongozi ambao haujali maslahi ya Tanzania Bara.

Wanachama hao walioongozwa na Kaimu Mwenyekiti Wilaya, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee Wilaya na Katibu wa Vijana wa Wilaya hiyo wamesema hawaoni umuhimu wa kuendelea kuitwa wanachama katika chama ambacho hakizingatii demokrasia na maslahi ya wengi.

Siyo kawaida kwa ofisi za vyama vya siasa kuwa zimefungwa wakati wa masaa ya kazi kwa kuwa wakati wowote zinapaswa kutoa huduma kwa wanachama wake.

Kwa CUF Wilaya ya Ilemela jambo hili limewezekana kwa kuwa hakuna tena kiongozi wa kuwasikiliza wanachama.

Madai ya kutokutolewa kwa ruzuku ya shilingi laki tatu kila mwezi ili kuendesha ofisi zilizoko wilaya 116TanzaniaBara kama ilivyoamriwa tangu Oktoba mwaka jana pamoja na kufukuzana uanachama ni miongoni mwa mambo yaliyowakera wanachama hawa hatimaye wakafikia uamuzi wa kujiengua.

Kwa mujibu wa Kaimu Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Ilemela Bwana Shaaban Itutu hawaoni sababu za kufukuzwa uanachama kwa Hamad Rashid Mohamed Mbunge wa wawi na wenzake kwa kuwa madaiyaoyalikuwa ni ya kuimarisha chama hicho.

Viongozi hawa pia wanaona chama chao kimevunja sheria namba 5 ya mwaka 1992 iliyoanzisha vyama vingi vya siasa ambavyo lengolakeni kuruhusu uhuru wa mawazo ambapo pia wanahofu juu ya serikali ya umoja wa kitaifa kuwa imedhoofisha chama chao.

Januari 3 mwaka huu viongoi hawa walitoa pendekezo kwa Baraza la chama hicho kutumia busara katika kuamua mustakabali wa Hamad Rashid Mohamed na wenzake ombi ambalo wanaliona kuwa lilipuuuzwa na hatimaye maamuzi ya kuwafukuza uanachama yakachukuliwa Januari 4.

           

Mwisho

Leave a Comment

More from category

Mgogoro CUF, Wananchi waendelea kujivua uanachama
Mgogoro CUF, Wananchi waendelea kujivua uanachama

Na Beatrice Ojjiki, Dar es Salaam.                               Chama cha wananchi CUF [Read More]

Wananchi walalamikia viongozi Gairo.
Wananchi walalamikia viongozi Gairo.

Na Kasilda Mlimila, Morogoro. Wananchi wa Gairo wilayani Kilosa, mkoa wa Morogoro wanakabiliwa na kero mbalimbali [Read More]

Ajali ya moto, Kiwanda cha samani za ndani chateketea Dar.
Ajali ya moto, Kiwanda cha samani za ndani chateketea Dar.

Na Faraji Mwagowa, Dar Es Salaam. MOTO mkubwa umezuka na kuteketeza kiwanda cha samani za ndani na baadhi ya maduka [Read More]

Chakula cha ziada, Hatua za dharura za muda mrefu zahitajika
Chakula cha ziada, Hatua za dharura za muda mrefu zahitajika

Na Joseph Mpangala,                                     Dar es Salaam. Mkutano wa [Read More]

Maeneo ya kimila ya kimasai, Ukuaji mji wa Monduli hatarini kuyapoteza.
Maeneo ya kimila ya kimasai, Ukuaji mji wa Monduli hatarini kuyapoteza.

Na Ramadhan Mvungi, Arusha.  Kasi ya kupanuka kwa Mji wa Monduli mkoani Arusha imetishia kutoweka kwa maeneo ya [Read More]