Wednesday February 22nd 2012

Mgomo wa madaktari, Morogoro nao wakumbwa wakati mgumu.

Na Kasilda Mlimila, Morogoro

Wakati huo huo, mgomo wa madaktari ulioanza Januari 24 mwaka huu katika hospitali ya taifa Muhimbili na kusambaa kwenye mikoa ya Dodomana Mbeya sasa umetua mkoani Morogoro baada ya madaktari wa hospitali kuu ya Mkoa kugoma na kusababisha tahaluki kubwa kwa wagonjwa.

Mgomo huo wa madaktari katika hospitali ya Mkoa umeanza mapema asubuhi ya Januari 26 ambapo kwa mujibu wa wagonjwa waliozungumza na Star Tv hospitalini hapo hakuna hata mgonjwa mmoja aliyepatiwa matibabu.

Wagonjwa hao wameiomba serikali kushughulikia madai ya madaktari ili waweze kusitisha mgomo na hivyo kuokoa maisha ya wagonjwa wengi waliopo hospitalini hapo ambao hali zao ni mbaya kutokana na kukosa matibabu.

Hata hivyo Star Tv ilipotaka kupata maelezo kutoka kwa uongozi hospitalini hapo kuhusiana na mgomo huo imeelezwa kuwa Mganga Mkuu wa Mkoa yupo safarini kikazi na viongozi wengine waliobakia katika hospitali hawakuwa tayari kuzungumzia lolote kuhusiana na mgomo huo.

Star Tv ilipowafuata madaktari waliokuwa katika mkutano kwenye moja ya majengo yaliyopo hospitalini hapo ili wazungumzie mgomo wao wamekataa katakata kuongea ama kupigwa picha.

 

Mwisho

One Comment for “Mgomo wa madaktari, Morogoro nao wakumbwa wakati mgumu.”


Leave a Comment

More from category

Mgogoro CUF, Wananchi waendelea kujivua uanachama
Mgogoro CUF, Wananchi waendelea kujivua uanachama

Na Beatrice Ojjiki, Dar es Salaam.                               Chama cha wananchi CUF [Read More]

Wananchi walalamikia viongozi Gairo.
Wananchi walalamikia viongozi Gairo.

Na Kasilda Mlimila, Morogoro. Wananchi wa Gairo wilayani Kilosa, mkoa wa Morogoro wanakabiliwa na kero mbalimbali [Read More]

Ajali ya moto, Kiwanda cha samani za ndani chateketea Dar.
Ajali ya moto, Kiwanda cha samani za ndani chateketea Dar.

Na Faraji Mwagowa, Dar Es Salaam. MOTO mkubwa umezuka na kuteketeza kiwanda cha samani za ndani na baadhi ya maduka [Read More]

Chakula cha ziada, Hatua za dharura za muda mrefu zahitajika
Chakula cha ziada, Hatua za dharura za muda mrefu zahitajika

Na Joseph Mpangala,                                     Dar es Salaam. Mkutano wa [Read More]

Maeneo ya kimila ya kimasai, Ukuaji mji wa Monduli hatarini kuyapoteza.
Maeneo ya kimila ya kimasai, Ukuaji mji wa Monduli hatarini kuyapoteza.

Na Ramadhan Mvungi, Arusha.  Kasi ya kupanuka kwa Mji wa Monduli mkoani Arusha imetishia kutoweka kwa maeneo ya [Read More]