Na Joseph Mpangala,
Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda amesema Serikali ipo katika mikakati ya kuhakikisha sekta ya kilimo inaboreshwa kwa kuwawezesha wakulima kuzalisha chakula cha ziada watakachokiuza na kujiongezea kipato.
Waziri Mkuu Pinda amebainisha mikakati hiyo kwenye mkutano wa siku mbili baina ya Wizara ya Fedha na Wadau wa Maendeleo unaojadili masuala ya Maendeleo na Uchumi.
Ingawa sekta ya kilimo inachukua asilimia 80 ya wananchi wote waTanzaniakwa kujishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na biashara lakini bado sekta hiyo haijapewa kipaumbele cha kutosha ili kumwezesha kila mwananchi anayejishughulisha na kilimo anufaike kikamilifu.
Akiongea mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa wadau wa maendeleo, Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda amesema ili kuhakikisha sekta ya kilimo inafanya vizuri ni lazima taasisi zisizo za kiserikali pamoja na Sekta binafsi kuhakikisha zinashiriki kikamilifu kwa kutoa mawazo na msaada wa kifedha kwa wakulima nchini.
Nao wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wanaoshiriki mkutano huo wamesema bila kutafuta soko la uhakika kwa wakulima wadogo pamoja uboreshaji wa miundombinu na nishati ya umeme kwa ajili ya kuhifadhia mazaoyaobado juhudi za kuwanua kiuchumi wakulima nchini zitaendelkea kukabiliwa na changamoto kubwa.
Hata hivyo wajibu wa Serikali unaonesha kuwa uboreshaji wa masoko ya mazao ya kilimo na biashara pamoja na uuzaji wa mazao kwa kutumia sayansi na teknolojia unatakiwa kuimarishwa kwa kuwaelimisha kabla ya kuuza bidhaa zao.
Mwisho










