Wednesday February 22nd 2012

Sudan: Marais wakutana Addis Ababa.

Marais wa Sudan Kusini na Sudan wanakutana mjini Addis Ababa, Ethiopia katika juhudi za kutafuta suluhu kwa tofauti zilizoibuka kati ya majirani hao wawili kuhusu mafuta.

Tangu kujitenga kwake kutoka kwa Sudan, Sudan Kusini imekuwa ikisafirisha mafuta yake kwa mauzo ya nje ya nchi kupitia mabomba ya Sudan.

Hata hivyo makubaliano ya kiwango cha malipo ya gharama ya uchukuzi hayakuafikiwa.

Sudan imelazimika kuchukua bila ruhusa mafuta hayo au kama inavyodai Sudan Kusini kuyaiba.

Kujibu vitendo hivyo Sudan Kusini ilitangaza kusitisha uzalishaji wa mafuta na kutengeneza bomba jipya la kusafirisha mafuta yake kupitia bandari ya Lamu nchini Kenya hatua ambayo huenda ikaathiri uchumi wa mataifa hayo mawili.

Ni kwa maana hii viongozi wa mataifa hayo mawili wanakutana.

Marais wa Kenya na Ethiopia wanaohudhuria mkutano huu watajaribu kuwapatanisha mahasimu hawa wa jadi. Inahofiwa kama hilo halitafanyika kutazuka mzozo mkubwa kati ya majirani hawa.

BBC

Leave a Comment

More from category

Gauck kuwa rais mpya wa Ujerumani
Gauck kuwa rais mpya wa Ujerumani

Viongozi wa kisiasa nchini Ujerumani wamemchaguwa mwanaharakati wa haki za binadamu Joachim Gauck kuwa mgombea wao wa [Read More]

Leo ni siku ya uchaguzi wa urais nchini Yemen.
Leo ni siku ya uchaguzi wa urais nchini Yemen.

Raia wa Yemen wanaamkia katika vituo vya kupigia kura kumchagua rais wao mpya, leo Jumanne. Wafuasi wa Abd Mansour Hadi [Read More]

Jeshi la Nigeria lawauwa Boko Haram.
Jeshi la Nigeria lawauwa Boko Haram.

Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kwamba wanajeshi watatu walijeruhiwa katika makabiliano hayo ya risasi na kundi la [Read More]

Libya sasa yashindwa kudhibiti wapiganaji
Libya sasa yashindwa kudhibiti wapiganaji

Shirika la kutetea haki za binadamu, Amnesty International linasema visa vya mateso, mauaji na watu kuzuiliwa bila [Read More]

Waziri avamia wapenzi wa jinsia moja.
Waziri avamia wapenzi wa jinsia moja.

Waziri mmoja nchini Uganda amevamia warsha ya wanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja na kujaribu kumkamata mwandaaji wa [Read More]