Wednesday February 22nd 2012

Ujenzi boya jipya la mafuta, mradi kukamilika mwezi Juni.

Na Christina Mbezi,                                       

Dar es Salaam.

Mradi wa Ujenzi na Uwekaji wa Boya Jipya la Mafuta yaliyosafishwa na yasiyosafishwa kwenye Bandari ya Dar es Salaam unatarajiwa kukamilika mwezi Juni kabla ya mradi huo kuanza kutumika rasmi Julai mwaka huu.

Mradi huo utakaogharimu Dola za Marekani Milioni 70 kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA na Benki ya Dunia ukikamilika unatarajiwa kuongeza uwezo wa kupakua mafuta kwenye bandari hiyo kutoka tani za ujazo 40,000 za sasa hadi tani 150,000.

Mradi huo uliotiwa saini Septemba 30 mwaka 2010 baina ya TPA na kampuni ya Leighton Offshore huko Singapore unahusisha utandazaji wa mabomba ndani na nje ya bahari na unatarajiwa kupunguza gharama za usafirishaji wa mafuta kwa kurahisisha upakuaji wake kwenye bandari ya Dar es Salaam, kupunguza msongamano wa meli zinazosubiri kupakua nishati hiyo na kuruhusu uingizaji wa meli kubwa tofauti na ilivyo hivi sasa.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Cassian N’gambo amesema hadi sasa ujenzi huo ulioanza Agosti mwaka jana umefikia zaidi ya asilimia Sitini.

Mradi huo utakapoanza rasmi mafuta yasiyosafishwa yanatarajiwa kupakuliwa kwa mita za ujazo wa 3,500 kwa saa na mafuta yaliyosafishwa yatapakuliwa kwa mita za ujazo wa 2,500 kwa saa.

Meli yenye tani 40,000 za nishati hiyo ikitarajiwa kupakuliwa kwa saa 20.

 

Mwisho

Leave a Comment

More from category

Zaidi ya magari 200 yakwama mpakani Holili
Zaidi ya magari 200 yakwama mpakani Holili

Na Enos Masanja, Moshi.  Zaidi ya magari 200 yanayosafirisha mzigo kupitia mpaka wa Holili juzi yamekwama kwa zaidi ya [Read More]

Zana za uchimbaji,  Wachimbaji Wadogo kunufaika kanda ya kati.
Zana za uchimbaji, Wachimbaji Wadogo kunufaika kanda ya kati.

Na Emmanuel Michael, Singida.  Wachimbaji wadogo wa madini ya aina mbalimbali kanda ya kati wanatarajiwa kuondokana na [Read More]

Umeme wa jua, Wakazi Kiagata Musoma kuanza kunufaika.
Umeme wa jua, Wakazi Kiagata Musoma kuanza kunufaika.

Na Mabere Makubi,             Musoma.  Wakazi wa vijiji 14 vya Tarafa ya Kiagata Wilaya ya Musoma vijijini [Read More]

Uwepo mgao wa umeme, Waziri wa Nishati na Madini akanusha.
Uwepo mgao wa umeme, Waziri wa Nishati na Madini akanusha.

Na Ivona Kamuntu, Mwanza.  Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja amekanusha kuwa hakuna mgao wa umeme [Read More]

Sekta ya Utalii Mwanza,  Miundombinu na uwanja wa ndege vikwazo
Sekta ya Utalii Mwanza, Miundombinu na uwanja wa ndege vikwazo

Na Rogers William,Mwanza.  Tatizo la miundombinu na ukosefu wa uwanja wa ndege wa kisasa katika jiji la Mwanza [Read More]