Wednesday February 22nd 2012

Ukanda wa kiuchumi baharini, kauli ya Prof. Tibaijuka yajadiliwa

Na Faraji Mwagowa,                                      

Dar es Salaam.

Kauli ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka kuwaZanzibarimeshirikishwa kikamilifu kwenye mchakato wa kuomba eneo la ziada nje ya Ukanda wa Kiuchumi Baharini limepokelewa kwa mitazamo tofauti na baadhi ya Wabunge.

Profesa Tibaijuka ametoa ufafanuzi huo kutokana na hatua ya Mwakilishi wa Mji Mkongwe Zanzibar Ismail Jussa Ladhu kuwasilisha hoja ya Dharura kwenye Baraza la Wawakilishi kwa madai kuwaZanzibarhaijashirikishwa kwenye mchakato huo na kutilia shaka maombi hayo kuwa hayana maslahi kwa Wazanzibar.

Wakizungumza na Star Tv jijiniDar es Salaam, baadhi ya Wabunge wamedai kuwa Wazanzibar wamekuwa wakitengwa katika maamuzi nyeti yanayogusa maslahiyaokwa kutumia mgongo wa Muungano.

Wamesema licha ya kwamba Katiba haijafuatwa katika sualahilopia hata elimu haijatolewa kwa Wazanzibar kuhusu mchakato huo.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa upande wa visiwani, Mbunge wa Singida Mashariki Mheshimiwa Tundu Lissu amesema umefika wakati kwa Watanzania kuacha kuuma maneno kwa kuwatamkia wenzao wa visiwani kwambaZanzibarsiyo nchikamaambavyo wamekuwa wakirubuniwa na baadhi ya Wanasiasa.

Kwa upande wake, Mbunge wa Simanjiro Mheshimiwa Christopher Ole Sendeka amesema hoja ya Wazanzibar ya kushirikishwa katika sualahilohaina mashiko kwa madai kuwa siyo kila jambo lazima wananchi wote washirikishwe.

Kauli hizo zinatokana na hatua ya hivi karibuni ya Waziri Tibaijuka kuongoza ujumbe wa watu kumi wakiwemo wawili kutokaZanzibarkwenda nchini Marekani kuwasilisha andiko laTanzaniakwenye Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuomba kuongezewa eneo la Bahari kwa maili 150 kwa ajili ya shughuli za kiuchumi zinazohusu mambo ya Bahari.

 

Mwisho

Leave a Comment

More from category

Zaidi ya magari 200 yakwama mpakani Holili
Zaidi ya magari 200 yakwama mpakani Holili

Na Enos Masanja, Moshi.  Zaidi ya magari 200 yanayosafirisha mzigo kupitia mpaka wa Holili juzi yamekwama kwa zaidi ya [Read More]

Zana za uchimbaji,  Wachimbaji Wadogo kunufaika kanda ya kati.
Zana za uchimbaji, Wachimbaji Wadogo kunufaika kanda ya kati.

Na Emmanuel Michael, Singida.  Wachimbaji wadogo wa madini ya aina mbalimbali kanda ya kati wanatarajiwa kuondokana na [Read More]

Umeme wa jua, Wakazi Kiagata Musoma kuanza kunufaika.
Umeme wa jua, Wakazi Kiagata Musoma kuanza kunufaika.

Na Mabere Makubi,             Musoma.  Wakazi wa vijiji 14 vya Tarafa ya Kiagata Wilaya ya Musoma vijijini [Read More]

Uwepo mgao wa umeme, Waziri wa Nishati na Madini akanusha.
Uwepo mgao wa umeme, Waziri wa Nishati na Madini akanusha.

Na Ivona Kamuntu, Mwanza.  Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja amekanusha kuwa hakuna mgao wa umeme [Read More]

Sekta ya Utalii Mwanza,  Miundombinu na uwanja wa ndege vikwazo
Sekta ya Utalii Mwanza, Miundombinu na uwanja wa ndege vikwazo

Na Rogers William,Mwanza.  Tatizo la miundombinu na ukosefu wa uwanja wa ndege wa kisasa katika jiji la Mwanza [Read More]