Na Zacharia Mtigandi,
Manyara.
Askofu mkuu wa kanisa la elimu pentekoste nchini mchungaji Peter Konkii ameiasa serikali kuchunguza kwa makini vyanzo vya vurugu mbalimbali zinazojitokeza wakati wa kampeni za chaguzi ndogo za vyama vya siasa hapa nchini.
Askofu huyo alitoa kauli hiyo mjini Babati mkoani Manyara kwenye misa ya pasaka ambapo pia aliitaka serikali kuhakikisha inasimamia vema chaguzi hizo ili ziendeshwe kwa amani na utulivu.
Alisema kuwa inasikitisha kuona katika kampeni hizo maisha ya watu yanakuwa hatarini kutokana na matukio mbalimbali ya uharifukamaalivyotolea mfano wapunge wawili walivyovamiwa na kupigwa jijini Mwanza hivi karibuni katika harakati hizo za kampeni.
Katika misa hiyo ya pasaka mchungaji msaidizi wa kanisahilola elimu Pentekoste mjini Babati Amani Michael anawasisitiza wakristo kusheherekea siku hii kwa kufanya matendo mema katika jamii.
Mwisho
No Comments