); bloginfo(

Mpwapwa wataka serikali tatu.

Na Fatma Gafus, Dodoma.      

BAADHI ya wakazi wa Wilaya ya Mpwapwa wametaka kuwepo kwa Serikali  tatu katika katiba mpya ambayo wanadai itakidhi matakwa ya watanzania walio wengi .

Wananchi hao walidai kuwa ni vyema Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar SMZ na Tanzania Bara kila moja iwe na katiba yake na kuwe na mamlaka kamili ya kiutawala.

Madai hayo yanakuja kufuatia mdahalo wa kujadili uundwaji wa katiba mpya ambao umefanyika wilayani humo na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya siasa na maendeleo pamoja na wanaharakati.Kelvin Haule ni mionginI mwa wanaharakati walioshiriki mdahalo huo

Mojawapo ya mambo yanayodaiwa kuikera jamii ni kitendo cha Rais kushindwa kuchukua maamuzi ya haraka pale anapopewa taarifa zenye ushahidi kuhusu matukio mbalimbali ya ubadhirifu na uvunjifu wa amani,hatua wanayoamini itapatiwa ufumbuzi kwa kiongozi huyo wa Nchi kupunguziwa mzigo wa madaraka.James Karayemala ni ni miongoni mwa washiriki.

Baadhi ya washiriki walisimama na kutoa maoni yao kuhusu uhalali wa Mbunge kuwa waziri hatua wanayoitazama kuwa ni sehemu ya kumfunga mdomo asipate fursa nzuri ya kuwatetea wapiga kura wake. 

Bibi Jane Mbelwa Mwanasheria katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa na Dokta Sinda Mussa Mhadhiri katika Chuo Kikuu ch a Dodoma UDOM ni  watoa mada.

Mdahalo huo wa kuwajengea uwezo  wananchi  waweze kutoa maoni yao kwa  Tume ya Rais ya kuratibu na kukusanya maoni ya uundwaji wa Katiba Mpya umeandaliwa na Mtandao wa Asasi za Kiraia wa Wilaya ya Mpwapwa na umefadhiliwa na Taasisi ya Foundation for Civil Society.

 

MWISHO.

VN:F [1.9.22_1171]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.22_1171]
Rating: 0 (from 0 votes)

No Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>