); bloginfo(

Uzalishaji mazo ya kilimo na biashara, Trekta kuongeza ufanisi Kahama.

Na Shaban Alley,

Shinyanga.

Baadhi ya wakulima wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamesema utumiaji wa trekta utaongeza ufanisi katika kilimo cha mazao ya chakula na biashara.       

Wakulima wa wilayani Kahama wamemwambia Waziri mkuu Mizengo Pinda kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia jembe la kukokotwa na ngombe katika shughuli zao za kilimo hali ambayo ilisababisha kupata mavuno kidogo.

Kwa mujibu wa wakulima hao, trekta hizo zitaongeza uzalishaji wa mazao hususani zao la dengu hali ambayo itainua uchumi wao.

Hivi sasa soko la zao la dengu limekuwa la uhakika ambapo kwa msimu wa kilimo uliopita gunia moja la kilo 120 liliuzwa kwa shilingi laki moja na elfu ishirini.

Meneja wa kampuni ya Ndegsela Bwana James Matonange amesema mazao ya biashara ya wakulima wa wilaya ya Kahama yamekuwa yakinunua kwa wingi na kampuni yake.

Naye Kaimu afisa kilimo wilayani Kahama Bwana Denis Samamba amesema halmashauri ya wilaya hiyo inaendelea na juhudi za kuhakikisha zana za kilimo zinapatikana.

Waziri mkuu alikuwa wilayani Kahama kwa ziara ya siku mbili na ameanza ziara yake mkoani Geita September 09, 2012.

VN:F [1.9.22_1171]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.22_1171]
Rating: 0 (from 0 votes)

1 Comment

  1. Gert says:

    That\’s a skillful answer to a difficult quseiton

    VA:F [1.9.22_1171]
    Rating: 0.0/5 (0 votes cast)
    VA:F [1.9.22_1171]
    Rating: 0 (from 0 votes)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>