); bloginfo(

Ukosefu wa umeme kikwazo wawa kikwazo kwa huduma ya mawasiliano.

Na Joyce Mwakalinga,                    

Dar Es Salaam.

Serikali bado inakabiliwa na changamoto ya kufikisha huduma za mawasiliano kwenye maeneo mengi ya vijijini kutokana na ukosefu wa umeme.

Hali hiyo ambayo imesababisha makampuni makubwa ya simu kushindwa kufika vijijini imebainishwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa mawasiliano ulifanyika jijiniDar Es Salaam.

Kutokana na hali hiyo, serikali imeanzisha mfuko wa mawasiliano kwa wote unaofadhiliwa na wadhamini na wadau mbalimbali.

Waziri mwenye dhamana husika na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema mfuko huo utasaidia kupunguza au kumaliza kabisa tatizohilo.

Kuhusiana na baadhi ya mitambo kutochimbiwa vizuri na kusababisha kupunguza ufanisi katika sekta hiyo Profesa Mbarawa anakiri kwa upande mmoja na kwa upande mwingine anabainisha jitihada wanazozifanya pindi yanapotokea mafuriko na kubomoa miundombinu hiyo.

Baadhi ya wadau wa mawasiliano wamewataka wadau wa sekta hiyo kutoka nchi mbalimbali kuja kuwekezaTanzania.

Awamu ya kwanza ya ukamilishaji wa mkongo wa taifa wa mawasiliano ilianza kutekelezwa Februari 2009 na kukamilika Juni 2010 wakati awamu ya pili ilianza kutekelezwa Agosti 2010 na kukamilika 2012.

Jumla ya kampuni 6 za nchini Tanzania zimeshajiunga katika mkongo huo, kampuni 6 za Rwanda na kampuni 2 zikijiunga kutoka Malawi na Kenya ikiwa katika mchakato huo.

VN:F [1.9.22_1171]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.22_1171]
Rating: 0 (from 0 votes)

No Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>