); bloginfo(

Zoezi la ukaguzi wa madereva walevi kuanzia na wanaoendersha magari ya abiria.

Na Nyanda Neema,

Dar es Salaam.

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dokta Emmanuel Nchimbi amesema zoezi la ukaguzi wa madereva wanaoendesha magari wakiwa wamekunywa pombe litaanzia kwa madereva wa magari yanayobeba abiria.

Waziri Nchimbi amesema hayo wakati akipokea vifaa maalumu kwa ajili ya kupima vilevi mwilini kutoka kampuni ya bia ya Serengeti SBL jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani.

Hadi sasa takwimu za ajali za barabarani zilizotokana na ulevi kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita kuanzia mwaka 2009 hadi 2011 niĀ 972 kati ya ajali zote 71, 390 katika kipindi hicho.

Waziri Nchimbi amesema katika kipindi cha miezi 6 ya mwaka 2012 ulevi umesababisha ajali 47 kati ya ajali zote 11,163 takwimu ambazo zinadaiwa kuwa ni chache lakini pengine niĀ kutokana na uhaba wa vifaa hivyo.

Kwa upande wake Teddy Mapunda Afisa Uhusiano wa SBL amesema kampuni yake imetoa msaada ya vifaa vya kupimia ulevi 20 vyenye thamani ya shilingi milioni 60 pamoja na nakala 20,000 za vitabu vya mafunzo ya utoaji wa leseni mpya.

Wiki ya nenda kwa usalama barabarani mwaka huu inatarajiwa kuanza Septemba 17 ambapo imeelezwa kuwa vipima ulevi hivyo vitasaidia utendaji wa jeshi la polisi kwa kuweza kuwabaini mapema madereva wanaoendesha magari wakiwa wametumia vilevi.

VN:F [1.9.22_1171]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.22_1171]
Rating: 0 (from 0 votes)

No Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>