Na Fredy Bakalemwa,
Mbeya.
Wanafunzi 70426 wameanza kufanya mtihani wa kumaliza darasa la Mkoani Mbeya kwenye shule za msingi 1025 kati ya 1081 zilizopo mkoani humo.
Hata hivyo idadi ya watahimiwa imepungua ikilinganishwa na mwaka jana ambapo walikuwa zaidi ya elfu 78,000.
Taarifa hiyo ilitolewa na afisa elimu mkoani hapa Juma Kaponda ambaye alisema wakati wa kupokea mtihani hiyo walipata tatizo la kalamu Kutokana na mfumo kubadilika na kutumika mfumo wa HB.
Wasimamizi wa mitihani hiyo ni 3160, ambao wamekula kiapo kuepuka udanganyifu ambao mwaka jana ulisababisha wanafunzi 216 kufutiwa matokeo
Nimepita kupita katika baadhi ya shule jijini Mbeya ambapo wanafunzi hawa baada ya kumaliza mitihani ya masomo ya kiingereza na hisababiti wamesema wamekumbana na ugumu katika mfumo mpya wa kujaza majawabu.
Wilaya ya Mbozi ndiyo wenye watahimiwa wengi 17051 huku wilaya ya Ileje ndiyo yenye idadi ndogo kiasi cha wanafunzi 4246 katika ya wilaya 8 za mkoa wa Mbeya.
No Comments