); bloginfo(

Utafiti wa Twaweza 2010, Hospitali za serikali zanyoshewa kidole.

Na Flora Mallya,

Dar es Salaam                    

Utafiti uliofanywa na shirika la TWAWEZA mkoani Dar es Salaam kwa mwaka 2010 umeonyesha rushwa na ucheleweshwaji wa huduma za afya ukiendelea kwenye hospitali na vituo vya afya vinavyomilikiwa na serikali.

Utafiti huo ulifanyika kwa miezi miwili na kushirikisha kaya 550 katika wilaya za Ilala, Temeke na Kinondoni.

Ripoti ya utaafiti huo, ilisomwa mbele ya waandishi wa habari huku ikionyesha  mpango wa serikali katika usambazaji wa vyandarua kwa kaya ulipata mafanikio ambapo asilimia 95 za kaya zina angalau chandarua kimoja.

Mtafiti Mchambuzi wa TWAWEZA Nyankomo Marwa anaasema utafiti huo, pia ulionyesha kaya moja kati ya tatu inauguliwa, huku watoa huduma za afya wakidai rushwa kutoka kwa wagonjwa.

Rakesh Rajan ni Mkurugenzi wa TWAWEZA, analazimika kutoa somo kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya rushwa pindi wanapokwenda kutibiwa.

Aidha, kuna uhitaji mkubwa wa huduma ya vituo vya afya vya serikali, ambapo asilimia 60 ya washiriki wanatumia vituo hivyo kwa ajili ya matibabu huku asilimia  82 ya watu wenye vipato vya chini wanatumia vituo vya afya vya serikali.

VN:F [1.9.22_1171]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.22_1171]
Rating: 0 (from 0 votes)

No Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>