Na Joyce Mwakalinga,
Dar Es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete amezindua rasmi mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni jijiniDar Es Salaam.
Daraja hilo linatarajiwa kuwa na urefu wa mita 680 na jumla ya njia sita, tatu zikielekea Kigamboni na nyingine tatu zikitokea Kigamboni.
Ujenzi wa daraja hilo utajumuisha barabara za maingilio ya daraja zenye jumla ya kilomita 1.5 upande wa Kigamboni na kilomita 1 upande wa Kurasini ikiwa ni pamoja na njia za watembea kwa miguu, baiskeli na pikipiki zenye upana wa mita 2.5 kila upande.
Rais Jakaya Kikwete ametumia fursa hiyo kuwataka wanasiasa kuacha kubeza maendeleo yanayofanywa na serikali kwani mafanikio hayo ni kwa maslahi ya taifa zima.
Waziri wa ujenzi Dokta John Magufuli amewataka wananchi walio pembezoni mwa maeneo ya ujenzi huo wasijenge ili kupisha ujenzi huo.
Amesisitiza kuhusiana na serikali kuwalipa fidia wale wote watakaoathiriwa na ujenzi huo kwa mujibu wa sheria.
Ujenzi wa darajahilounagharimiwa na serikali yaTanzaniaambayo itachangia asilimia arobaini kwa kushirikiana na shirika la Taifa la hifadhi ya jamii NSSF ambalo litachangia asilimia 60 ya gharama ya mradi.
Ujenzi huo unaotarajiwa kutumia jumla ya shilingi bilioni 214.6 utakamilika katika muda wa miezi 36 kuanzia Februari 2012 ambapo watembea kwa miguu na watumiaji wa baiskeli watalitumia bila malipo yoyote.
Daraja linajengwa na kampuni ya China Railway Construction Engineering Group ambayo inashirikiana na kampuni ya China Major Bridge Engineering.
No Comments