Na Denice Mwasalanga,
Dar es Salaam.
Kamati ya Bunge ya haki, maadili na madaraka ya Bunge imeonya vyombo vya habari, wanasiasa na watendaji wa serikali kuendelea kujadili suala lililoibuliwa Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuhusiana na uteuzi wa majaji wa mahakama kuu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kamati hiyo imesema sualahilolinafanyiwa uchunguzi wa kina hivyo kuendelea kulijadili ni uvunjifu wa kanuni na utaratibu zilizowekwa kisheria.
Taarifa ya kamati hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ya kudumu ya haki, maadili na madaraka ya Bunge Brigedia Jenerali Mstaafu Hassan Ngwilizi kutokana na malumbano ambayo yaliibuliwa Bungeni Julai 13 mwaka huu wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2012/13.
Kamati hiyo imetoa ufafanuzi huo baada ya hivi karibuni kuibuka malumbano kupitia baadhi ya vyombo vya habari na baadhi ya taarifa kurejea kinachosemekana kutokea ndani ya kamati hiyo.
Kutokana na sintofahamu hiyo kamati imesema imechukua hatua kwa wahariri wa vyombo vya habari kadhaa ambavyo vimeripoti habari kinyume na sheria wakati kamati haijakamilisha kazi yake.
Vyombo hivyo vya habari vinavyofanya kazi kwa mujibu wa ibara ya 18 ya katiba, licha ya kutotajwa majina kwa kujadili taarifa ambazo zipo ndani ya kamati vimeelezwa kuwa vimeenda kinyume na kifungu cha 31 (1) (F) cha sheria haki, kinga na madaraka ya Bunge, sura 296.
Kamati ya Ngwilizi imekumbushia mwongozo uliotolewa na Mbunge Gosbert Begumisa Blandes ambaye alitaka ufafanuzi kuhusiana na kauli ya Kiongozi wa kambi ya upinzani kuwa amedhalilisha majaji na alitaka mwongozo kuhusu taratibu za bunge kujadili mhimili wa mahakama.
Kufutia tamko la Mheshimiwa Lissu ombi la mwongozo kama ulivyotolewa na Blandes, baada ya maelekezo mengine ya kikanuni za bunge kamati ya haki na maadili iliagizwa ili ipitie mwenendo shughuli yote ya Julai 13 katika suala hilo kama inavyoonekana katika taarifa za Bunge yaani Hansard na kulishauri Bunge zima kwa ujumla wake hatma ya kufanya katika jambo hilo.
Tume hiyo ikikamilisha taarifa yake itaiwasilisha katika Bunge la jamuhuri ya muungano ambapo majibu yatapatikana.
No Comments