); bloginfo(

Soko la Sabasaba Dodoma lavunjwa, Mali za sh. mil. 500 zaharibiwa

Na Faraji Mwagowa,     

Dodoma. 

Mali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500 zimeharibiwa katika soko la matunda na mbogamboga sabasaba mjini Dodoma baada ya vibanda vya wafanyabiashara takribani 600 kuvunjwa usiku wa manane na wanaodhaniwa kuwa askari wa manispaa.

           

Tukio hilo linadaiwa kuwaacha katika taharuki, simanzi na huzuni wafanyabiashara hao huku lawama nyingi zikielekezwa kwenye uongozi wa manispaa hiyo.

           

Wakizungumza mapema asubuhi wafanyabiashara hawa wanadai tukio hilo limefanywa usiku wa manane kutokana na ukweli kuwa halikuwa na uhalali wa kisheria kwani manispaa ndiyo iliyowapa eneo hilo kwa matumizi ya kibiashara.

Kamera ya Star Tv imeshuhudia vibanda vya biashara, mbogamboga, matunda pamoja na mali nyingine vikiwa vimeharibiwa vibaya hali inayotafsiriwa kuwarudisha nyuma kimaendeleo waathirika wa tukio hilo baada ya kubainika kuwa wengi wao wanategemea mikopo kuendesha biashara zao.

Kufuatia hali hiyo Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara wa soko hilo Athuman Makole anasema hatua hiyo haina budi kulaaniwa vikali na jamii kwani imekiuka makubaliano ya awali kati ya uongozi wa soko na ule wa manispaa.

Tukio hilo linadaiwa kufanyika chini ya ulinzi mkali huku risasi za moto zikidaiwa kurushwa ovyo hewani kwa lengo la kuwatawanya baadhi ya raia walioanza kujongea kwenye eneo la tukio kwa kudhani kuwa huenda majambazi wapo kazini.

Juhudi za kuwapata viongozi wa manispaa hazikuweza kufanikiwa kutokana na wengi wao kuwa katika mapumziko ya mwisho wa wiki huku simu zao nazo zikiwa zimezimwa.

VN:F [1.9.22_1171]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.22_1171]
Rating: -1 (from 1 vote)

3 Comments

  1. Ezekiel says:

    Kama walikuwa hatataki kuhamisha biashara mngetangaza kwenye radio,tv,magazeti na hata tovuti ya serikali. Na zoezi lingefanyika mchanap,je milion 500 ni chache kuliko gharama ya matangazo? Mhusika achukuliwe hatua na umoja wa wafanya biashara afikishwe mahakamani. Poleni sana ndugu zangu kwa hasara mliyoipata.

    VA:F [1.9.22_1171]
    Rating: 0.0/5 (0 votes cast)
    VA:F [1.9.22_1171]
    Rating: 0 (from 0 votes)
  2. Kwanza nyie viongozi wa jiji, mliwanufaisha ‘migambo’ kwa kunyofoa visivyo wahusu(mboga). Na tuwajuavyo hao njaa kali!

    VA:F [1.9.22_1171]
    Rating: 0.0/5 (0 votes cast)
    VA:F [1.9.22_1171]
    Rating: 0 (from 0 votes)
  3. Uongozi wa manispaa ya Ddm haujawatendea haki wananchi wk! Kwanza ni kosa kubomoa usiku wa manane!. Ni kutojihamini.

    VA:F [1.9.22_1171]
    Rating: 0.0/5 (0 votes cast)
    VA:F [1.9.22_1171]
    Rating: 0 (from 0 votes)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>