I
I
I
I
I
Startv Tanzania-Habari
Copyright  @  STAR TV LTD . All Rights Reserved.
 
ZAIDI ya tani 360 za mpunga zimehifadhiwa na wakulima wa mpunga wa Kijiji cha  Madibira,Wilaya ya Mbarali chini ya programu ya mpango wa uendelezaji wa mifumo ya masoko ya mazao ya kilimo gharani kanda za nyanda za juu kusini ambao walipatiwa mkopo wa zaidi ya Sh .milioni 35 kutoka benki  ya wananchi ya Mufindi (MKOBA).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Mratibu msaidizi wa programu hiyo Bw. Aberhard Mbepera amesema kuwa programu hiyo imeanza kuwawezesha wakulima wa nyanda za juu kusini kujua namna ya kuhifadhi mazao katika maghara wakati wanasubiri bei za mazao kupanda ambayo itawafanya wakulima hao kupata faida.

Amesema kuwa Wilaya zingine ambazo wamewawezesha katika mpango huo ni Kyela, Kamsamba-Mbozi , na kwamba katika Wilaya ya Kyela wameweza kuhifadhi tani 120 za mpunga.

Aidha amesema kuwa zoezi hilo linaendeshwa na kutarajia msimu wa mwezi wa 12 ambapo wakulima watauza mpunga wao kwa bei ya nzuri ya  sh.450 kwa kilo.

Amesema kuwa bei ya mpunga kwa sasa ni sh.290 mpaka 300  ambayo haimpi mkulima faida na kuamua kuuza kwa hasira ili mazao yao yaweze kutoka kwa haraka .

Hata hivyo Bw. Mbepela amesema programu hiyo inakabiliwa na uhaba wa maghara ya kuhifadhia mazao katika Wilaya na mikoa na kwamba hata maghara yaliyopo hayana ubora wa uhakika ambayo yataweza kuhifadhi mazao ya wakulima hususani maeneo ya vijijini.

Amesema tatizo lingine ni ucheleweshaji wa fedha kutoka kwa taasisi zinazotoa mikopo kwa wakulima kusababisha wakulima wachache kujiunga kwenye mfumo wa stakabadhi za mazao vijijini na kwamba ili kuweza kukabiliana na hali hiyo programu imeanza kutoa elimu kwa wakulima kuhusiana  na faida za mfumo wa stakabadhi na kumfanya mkulima kuhifadhi mazao yake wakati akisubiri bei nzuri.

“Ili kuweza kujikomboa na tatizo hili tumeanza kufanya mikutano kwa  kutoa elimu  kuwashirikisha wakulima wenyewe,saccos na mabenki ambayo yanashughulika na kutoa mikopo ili tuweze kupunguza vikwazo wakati taasisi zikiwapatia mikopo wakulima wetu,” amesema Mratibu huyo.






.

. .




 
 
Programme Line Up