Home     I    About Us     I     Contact Us    I      Startv Crew    I     Schedule     I     Coverage     I     Login
Copyright  @  STAR TV LTD . All Rights Reserved.
Hayo yameelezwa jana usiku na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Balozi Msuya W. Mangachi wakati akitoa taarifa ya ubalozi huo kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye amewasili jana jijini Abuja, Nigeria kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi unaojadili masuala ya Viwanda na Usindikaji Mazao ya Kilimo barani Afrika unaofanyika kesho (Jumatano, Machi 10, 2010) katika hoteli ya Transcorp Hilton, jijini Abuja.

 

Balozi Mangachi alimweleza Waziri Mkuu kwamba idadi hiyo inahusisha wale waliochukulia viza ubalozini tu kwani kuna wengine ambao hupata viza wanapowasili nchini.

 

Alisema kama nchi, Nigeria inakabiliwa na changamoto nyingi hususan katika nyanja ya kisiasa kutokana na machafuko ya mara kwa mara jambo ambalo limeifanya demokrasia katika nchi hiyo kudumaa.

 

Alisema juhudi zinazofanywa hivi sasa na viongozi wa nchi hiyo zinaonyesha mafanikio na kwamba muda si mrefu nchi hiyo itachukua nafasi yake kama nchi moja muhimu katika bara la Afrika na katika jumuiya ya nchi zilizoendelea.

 

“Nigeria ni nchi tajiri kwa rasilmali watu na rasilmali za kiuchumi, endapo juhudi za viongozi za kuleta usimamizi bora wa rasilmali watu zitafanikiwa, Nigeria inaweza kuwa miongoni mwa nchi 20 zilizoendelea (G20) katika miaka michache ijayo,” alisema.

 

Alisema kuna haja ya kufufua Tume ya Pamoja ya Ushirikiano baina ya Nigeria na Tanzania (Joint Permanent Commission –JPC) na kuanzisha ushirikiano baina ya vyama vya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili (Chambers of Commerce) ili kuimarisha uhusiano wa kiuchumi wa nchi hizo.

 

Leo mchana Waziri Mkuu atatembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo jijini Abuja na kesho mchana (Jumatano, Machi 10, 2010) Waziri Mkuu atahutubia katika mkutano huo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ambapo wakuu wa nchi wamepewa nafasi kuzungumza.










.
Bongo Beats every Monday to Saturday @ 1900hrs
Bonga na Startv every  Monday to Saturday @ 1705hrs
Habari every  Monday to Sunday @ 2000hrs
Home                                            About Us                                                    Contact Us                                                Startv Crew                                           Login
Leo::
Startv Menu