Copyright @ STAR TV LTD . All Rights Reserved.
Hayo yameelezwa katika risala ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani,kiwilaya yaliyofanyika katika kata ya Sima wilayani hapa.
Akisoma risala hiyo mbele ya mgeni rasmi waziri wa Nishati na Madini Mh.Wiliamu Ngeleja,mwalimu Tumaini Masamu wa Sule ya msingi Sima ameeleza kuwa mikopo hiyo itawawezesha wanawake kuongeza kipato kwa njia ya kukopeshana katika shughuli mbalimbali za biashara na uzalishaji mali.
Wanawake hao wametumia fursa hiyo kuipongeza serikali na halmashauri ya wilaya ya Sengerema kwa kuanzisha mfuko wa maendeleo ya wanawake ili kuwaongezea vipato katika shughuli zao.
Aidha wameitaka serikali na masirika mbalimbali kufanya jitihada kuhusu kutatua kero zinazowakabili wanawake, kupiga vita mila na desturi zilizopitwa na wakati,kuzirekebisha sheria mbalimbali zinazomnyanyasa na kumkandamiza mwanamke,na kuongeza mikopo zaidi ili kumpa uweze wa kuongeza kipato na kuondokana na umasikini.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo,waziri Ngeleja amewataka wanawake kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi hasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuwataka kuacha kubaguana katika mchakato mzima wa uchaguzi.
Lengo la maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ni kutoa fursa mwanamke kwa serikali ili kuleta ukombozi na ushikamano na kuondoa mfumo dume unaochangia unyanyasaji wa wanawake.
Kauli mbio ya mwaka huu ni miaka 15 baada ya mkutano wa Beijing wanawake wanaweza,wapewe nafasi
Bongo Beats every Monday to Saturday @ 1900hrs
Bonga na Startv every Monday to Saturday @ 1705hrs
Habari every Monday to Sunday @ 2000hrs