I
I
I
I
Startv Tanzania-Habari
Home     I    About Us     I     Contact Us    I      Startv Crew    I     Schedule     I     Coverage     I     Login
Copyright  @  STAR TV LTD . All Rights Reserved.
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Pwani Laurent Ndalichako alisema makada hao walikamatwa usiku juzi wakiwa na bidhaa mbalimbali, zilizohifadhiwa vema katika vifurushi vitu ambavyo  moja kwa moja vinaashiria kulikuwepo na dhana nzima ya kutoa rushwa.

Amesema watuhumiwa hao wa rushwa walipotakiwa kueleza walizipata wapi, waliwataja baadhi ya wagombea kuwa ndio waliowapa kwa lengo la kuwashawishi wawapigie kura.

Ndalichako ametaja vifurushi walivyokamatwa navyo wapiga kura hao, kila kimoja kilifungasha jozi moja ya kitenge, jozi moja ya msala yaani mikeka ya kusalia, jozi lingine lilikuwa la nguo za kina mama maarufu kwa jina la madela.

Ametaja majozi mengine kuwa zilikuwa na vitambaa vya kufutia jasho maarufu enkachifu, mikoba ya kina mama pamoja na fedha taslimu sh. 72, 000.

Amesema waliokamatwa ambao hakutaka kuwataja kwa kile alichodai kuvuruga uchunguzi ni kutoka kata za Magindu, Ruvu, Kwala, Mlandizi, Pangani, Misugusugu,  na Mkuza.

Amesema maofisa wa taasi yake katika kipindi hiki cha uchaguzi wamesambaa kila pembe ya mkoa wa Pwani wakiwasaka na kuwatia nguvuni wale wote watakaobambwa wakitoa na kupokea rushwa.

MWISHO
Bongo Beats every Monday to Saturday @ 1900hrs
Bonga na Startv every  Monday to Saturday @ 1705hrs
Habari every  Monday to Sunday @ 2000hrs
Home                                            About Us                                                    Contact Us                                                Startv Crew                                           Login
Leo::
Startv Menu